Wababe wa Young Africans kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Jumapili (April 25) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Azam FC wameendelea kusisitiza kauli mbiu yao ‘TUNA JAMBO LETU’ msimu huu 2020/21.

Azam FC wamesisitiza kauli mbiu hiyo, baada ya kuaambulia alama tatu muhimu mbele ya Young Africans, kwa bao lililofungwa na mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe Prince Dube, na kufanikiwa kufiksha alama 54 zinazowaweka kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mkuu wa Idara ya Habari Na Mawasilino ya Azam FC, Zakaria Thabit ‘Zaka Zakazi’ amesema mipango waliyonayo bado inawapa nafasi ya kuamini kwamba jambo lao linakwenda kutimia.

“Huu ni mchezo wa mpira na inaonesha kwamba mzunguko wa pili ushindani ni mkubwa, ikiwa ipo hivyo basi hakuna namna kusema kwamba hatuna nafasi ya kutimiza jambo letu.

“Ukiwatazama wale wanaoongoza ligi wametuzidi pointi nne na wana mechi mkononi, sawa hilo lipo wazi ila nasi pia bado tuna mechi za kucheza hivyo tukishinda zetu wao wana kazi pia ya kupambana kushinda mechi zao.

“Kwa maana hiyo bado mbio za ubingwa zipo wazi na jambo letu tunaamini kwamba linakwenda kutimia kwa kuwa timu imerejea kwenye ule ubora wa awali,” amesema.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ilianza mzunguko wa kwanza kwa kufanya vizuri ambapo iliongoza ligi mpaka raundi ya 7 kisha hapo mambo yalianza kubadilika taratibu na kuwa kwenye mwendo wa kusuasua.

Kwa sasa ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 28 ina pointi 54, kinara ni Simba SC mwenye pointi 58 na amecheza jumla ya mechi 24, nafasi ya pili ipo mikononi mwa Yanga wenye pointi 57 baada ya kucheza mechi 27.

ASFC: Young Africans waifuata Tanzania Prisons
Waziri Ummy: Wazembe watupishe