Vinara wa Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC leo wataendelea na harakati za kulisaka taji la VPL, kwa kupambana na Mwadui FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam majira ya saa 1:00 usiku.

Azam FC wanakwenda kwenye mchezo huo, wakiwa na alama 15 walizozikusanya kwenye michezo mitano iliyopita ya VPL, huku wapinzani wao Mwadui FC wakiwa na alama 6, zinazowaweka katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Azam FC wametoa taarifa kuelekea mpambano huo, kwa kusema wapo tayari kupambana na kuendeleza wimbi la ushindi kama walivyofanya kwenye michezo mitano iliyopita.

Mkuu wa Idara ya Habari Na Mawasilino Wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu jijini Dar es salaam, Thabit Zacharia (Zaka Zakazi), amesema kikosi chao kipo tayari, baada ya kufanya maandalizi kwa siku kadhaa zilizopita.

“Hatuna majeruhi, tumejipanga vizuri na hivi sasa tunawasubiri wachezaji wengine, Yakubu Mohamed na Nicolaus Wadada ambao walikuwa kwenye majukumu yao kwenye timu zao za taifa,” amesema Zaka.

Mchezo mwingine wa mzunguumko wa sita unaochezwa leo Oktoba 15, Gwambina FC iliyo nafasi ya 14 itapambana Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 12.

Polisi kuwasaka waliowavamia Wagombea CHADEMA
Juventus FC yalazimika kujitenga