Uongozi wa Azam FC, umeweka wazi kwamba, kwa sasa unapunguza wachezaji ambao mikataba yao inamalizika na wengine ambao hawapo katika mipango ya msimu ujao, huku wakiwaongezea mikataba baadhi ya nyota, kisha suala la kushusha majembe mapya, likifuatia.

Tayari Azam FC imetangaza kuwaongezea mikataba Sospeter Bajana, James Akaminko na Nathaniel Chilambo, huku ikiachana na Wilbol Maseke, Agrey Morris, Rodgers Kola, Ismail Aziz Kader, Cleophace Mkandala, Keneth Muguna na Bruce Kangwa.

Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe, amesema: “Tunakuja na kishindo kwenye usajili wetu, hatuna jambo dogo kwani ipo wazi timu kubwa inafanya mambo makubwa nasi tupo kwenye orodha ya timu kubwa.

“Ripoti inatoa maelekezo ya nini kifanyike kwa sasa na hicho kinafanyika taratibu na kwa umakini, mashabiki imani iendelee kuwepo mambo mazuri yanakuja.

“Muhimu kuwa na subira na kuendelea kuwa pamoja na timu kwenye nyakati zote kisha tutakuwa imara kwenye mapambano.”

Inawezekana, usikatishwe tamaa na chochote - Anna
Kylian Mbappe aivuruga Paris Saint-Germain