Wachezaji wa timu ya Azam FC wakifanya mazoezi ya nguvu leo asubuhi kwenye Uwanja Azam Complex kujiandaa na mchezo dhidi ya African Sports utakaofanyika Jumamosi ijayo katika uwanja huo Azam Complex jijini Dar es salaam.

Benchi la Ufundi la Azam FC leo liliwapa mazoezi ya ufiti kidogo wachezaji kabla ya kuhamia kwenye mazoezi ya mbinu za uwanjani kuelekea mchezo huo.

Mara baada ya mazoezi hayo wachezaji waliingia moja kwa moja kambini tayari kwa maandalizi ya mchezo huo dhidi ya timu inayoshika mkia kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) wakiwa na pointi saba huku Azam FC ikiwa kileleni kwa pointi 35.

TFF Wakosa Nafasi Ya Kumpongeza Mchezaji Bora Wa Afrika
Joto La Usajili Wa Dirisha Dogo Laendelea Kupanda