Saa chache baada ya kuzindua Nembo Mpya ya klabu ya Azam FC katika hafla maalum iliyofanyika jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo Thabit Zakaria (Zaka Zakazi) ametoa ufafanuzi wa kina kupitia kauli iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Kwa kutumia akaunti zake binafsi za mitandao ya kijamii Zaka ameweka taarifa hiyo: KWA NINI MABADILIKO YA NEMBO?

Nembo ni kitu muhimu sana katika utambulisho wa taasisi yoyote.

Inavutia watu kukufuatilia kwa umakini na kwa ukaribu zaidi.

Husaidia kutengeneza ushawishi wa haraka kwa mtu anayekiona kitu kwa mara kwanza yaani first impression.

Ni msingi mkuu wa utambulisho wa jina chapa yaani brand.

Hukutenganisha na washindani wako kibiashara.

Hutengeneza uaminifu kwa chapa yaani brand kwa wafuasi wake.

Kama klabu, sisi Azam FC tumezingatia yote hayo katika kufikia maamuzi ya kuja na nembo hii ambayo tumeizindua.

Wakati tukiwa katika mradi mpya kuelekea msimu mpya na misimu mingine mbele, ni matarajio yetu nembo hii itatusadia kutujengea taswira mpya na matumaini mapya.

Ahsanteni sana

-Mtendaji Mkuu wa @azamfcofficial ndugu @abdulkarim.amin aka Popat

TFF: Ruhsa kusajili wachezaji 12 wa kigeni
Hans Poppe: Simba SC imekamilika kila idara