Klabu ya Azam FC imefanya mabadiliko ya uongozi kwa kumteua Nassor Idrissa Mohamed ‘Father’ kuwa Mwenyekiti, akichukua nafasi ya Shani Christoms.

Taarifa iiyotolewa na klabu hiyo imethibitisha mabadiliko hayo yaliyopewa baraka na Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC Ltd, huku mwenyekiti mpya Nassor Idrissa Mohamed akianza kazi rasmi tangu jana Jumanne (Januari 19).

Kabla ya uteuzi huu, Nassor Idrissa Mohamed, alikuwa akihudumu kama mkurugenzi mshauri wa Azam FC, na Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC Ltd, ina imani kubwa na mwenyekiti huyo mpya katika kufanya kazi yake ipasavyo, na kuipeleka mbali kimafanikio Azam FC.

Hata hivyo taarifa hiyo imetoa ufafanuzi wa kuondolewa kwa  Shani Christoms kwenye nafasi ya mwenyekiti, ambayo ameihudumu kwa zaidi ya miaka miwili.

Mamuzi hayo yamekuja kwa lengo la kumpa nafasi Shani kupata muda wa kutosha wa kujikita zaidi katika majukumu yake ya Mkurugenzi wa Sheria na Utawala wa Said Salim Bakhresa & Co.Ltd.

Rwanda yarejea 'lockdown' tena
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 20, 2021