Kikosi cha mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC, hii leo kimeelekea visiwani Zanzibar (Unguja) kwa ajili ya kambi ya juma moja ya kujiandaa na msimu ujao (2016/2017).

Kikosi cha Azam FC kimefikia katika Hoteli ya Kitalii ya Mtoni Marine, ambapo kikiwa visiwani Zanzibar (Unguja) kinatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki itakayotangazwa hapo baadaye.

Mchezo wa kwanza kwa mabingwa hao, umepangwa kufanyika Jumatano Ijayo na mwingine Jumamosi kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili ijayo.

TANAPA Yaipiga Tafu Timu Ya Taifa Ya Riadha
Chid Benz aeleza jinsi alivyomtoa machozi Mr Blue