Kocha Msaidizi wa Azam FC Vivier Bahati amesema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa ‘JKT Tanzania’.

Azam FC watakua wageni kwenye mchezo huo, utakaochezwa jijini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri Aprili 16, kuanzia mishale ya saa 8:00 mchana.

Kocha Bahati amesema maandalizi yanakwenda vizuri na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ujao na maandalizi yanakwenda sawa hivyo ni suala la kusubiri na kuona.

“Ushindi ni jambo ambalo tunalihitaji hivyo kwa morali ambayo wanayo wachezaji tunaamini kwamba tutafanya vizuri,”

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza michezo 25 ina alama 47 inakutana na JKT Tanzania yenye alama 27 ipo nafasi ya 12.

Mjumbe Simba SC afunguka mchakato wa mabadiliko
Onyango: Mapambano yanaendelea VPL

Comments

comments