Klabu ya Azam FC imemsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka Kenya Kenneth Muguna, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Gor Mahia.

Mkataba wa pande hizo mbili, utafikia kikomo mwaka 2023, huko Azam Complex Chamazi nje kidogo ya jiji l Dar es salaam yalipo makao makuu ya klabu hiyo.

Azam FC imethibitisha usajili wa kiungo huyo leo mchana, baada ya kuweka taarifa kenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Usajili wa Muguna anatarajia kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Azam FC katika eneo la ushambuliaji.

Miguna ni miongoni mwa nyota wanaotamba kwenye soka la Kenya, msimu huu alifanikiwa kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Kombe la FA la nchini humo, huku timu yake ya Gor Mahia ikiibuka mabingwa wa michuano hiyo.

Huu ni usajili wa nne kwa Azam FC katika kipindi hiki cha kuelekea msimu ujao, baada ya awali kuwasainisha nyota wawili kutoka Zambia, Charles Zulu, Rodgers Kola na beki wa kushoto Edward Manyama.

Naibu Waziri: TCRA, UCSAF kufikia agosti 16 muwe mmepata sululisho
NEMC yafanya ziara mradi wa uraniam