Uongozi wa Azam FC umetoa kauli kuhusu tetesi za Kiungo wa klabu hiyo Salum Abubakar ‘Suare Boy’ kuhusishwa na mpango wa kuwa mbioni kusajiliwa Young Africans.

‘Sure Boy’ anayetumikia adhabu ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana huko Azam Complex Chamazi, anatajwa kuwa kwenye mpango mkali wa kusajiliwa na ‘WANANCHI’ wakati wa Drisha Dogo la Usajili, ambalo rasmi litafunguliwa Desemba 15.

Akizungumzia jambo hilo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC, Zakaria Thabiti ‘ZAKA ZAKAZI’ amesema taarifa za mchezaji huyo kuwa mbioni kusajiliwa Young Africans wanaziona kwenye mitandao ya kijamii, lakini hazijawafikia rasmi mezani kwao.

Amesema Azam FC haina hiyana yoyote katika suala la kumuachia mchezaji anayehitajiwa na klabu nyingine, lakini akasisitiza kufuatwa kwa taratibu za uhamisho ambazo zinatambulika duniani kote.

“Sisi hatumzuii mchezaji yeyote kusajiliwa na timu nyingine, kikubwa timu husika inahitajika kufuata taratibu za usajili.” amesema ZAKA ZAKAZI.

Sure Boy alisimamishwa na Azam FC mwanzoni mwa msimu huu kwa utovu wa nidhamu, sanjari na wachezaji Mudathir Yahya na Agrey Morris.

Simba SC yaivaa Bodi ya Ligi TPLB
Sure Boy anukia Young Africans