Kocha kutoka nchini England, Stewart John Hall usiku wa kuamkia hii leo aliiongoza Azam FC kushinda mchezo wake wa 10 mfululizo tangu aliporejea klabuni hapo kwa mara ya tatu mwezi Juni mwaka huu, baada ya kuifunga KMKM 1-0 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Bao pekee la Azam FC katika mchezo huo lilifungwa na beki Gardiel Michael Kamagi Mbaga, kwa shuti la umbali wa mita 14 baada ya pasi ya Ramadhani Singano ‘Messi’.

Akiichezea kwa mara ya kwanza Azam FC tangu ahamie kutoka Simba SC mwezi uliopita, Ramadhan Singano “Messi” alionyesha kiwango kizuri kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC utakaochezwa Agosti 22, kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

TANGU AREJEE AZAM FC JUNI 2015

Azam FC 4-2 Friends Rangers (Kirafiki Chamazi)

Azam FC 1-0 JKT Ruvu (Kirafiki Chamazi)

Azam FC 1-0 African Sports (Kirafiki Tanga

Azam FC 1-0 Coastal Union (Kirafiki Tanga)

Azam FC 1-0 KCCA (Kagame Taifa)

Azam FC 2-0 Malakia (Kagame Taifa)

Azam FC 5-0 Malakia (Kagame Taifa)

Azam FC 0-0 Yanga SC (pen5-3, Robo Fainali Kagame Dar)

Azam FC 1-0 KCCA (Nusu Fainali Kagame Dar)

Azam FC 1-0 KMKM (Kirafiki Zanzibar)

 

Azam FC imeweka kambi Zanzibar kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wiki ijayo.

Wapinzani wao, Yanga SC wameweka kambi Tukuyu, Mbeya na jana walikuwa wana mchezo wa kirafiki, ambao wameshinda bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mabao ya Yanga katika mchezo huon yalifungwa na Malimi Busungu pamoja na Hamis Tambwe.

 

Ni Ronaldo, Messi Na Suarez 2015
Ray Awaonya Wasanii Na Siasa Za Tanzania, Awataka Wamchague Huyu..