Wawakilishi wa Tanzania kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Azam FC wameshindwa kufurukuta katika Uwanja wao wa nyumbani, baada ya kuambulia sare ya 0-0 dhidi ya Pyramids FC ya Misri.
Azam FC wamecheza katika kiwango cha kawaida kwenye mchezo huo uliounguruma Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Da es salaam, huku wachezaji wa Pyramids walionyesha uzoefu mkubwa wa kuhimili mbinu za wenyeji wao.
Hata hivyo umahiri wa mlinda lango wa Azam FC Mathias Kigonya umekua chachu ya Azam FC kupata matokeo ya sare nyumbani.
Azam FC italazimika kusaka ushindi kwa namna yoyote ikiwa ugenini nchini Misri mwishoni mwa juma lijalo.
Halikafhalika kwa upande wa Pyramids FC nao watalazimika kusaka ushindi katika mchezo wa Mkondo wa Pili utakaochezwa nyumbani kwao nchini Misri.