Uongozi wa Azam FC umetoa sababu za kusitisha mkataba wa kocha kutoka nchini Romania Aristica Cioaba, kwa kusema kucheza chini ya kiwango kwa timu yao katika michezo kadhaa ndio sababu kuu.

Azam FC walithibitisha kusitisha mkataba wa kocha huyo jana Alhamis jioni kupitia kwa Afisa Habari Zakaria Thabit, ambaye alisema mchakato umefanyika kuanzia timu ilipopoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar na michezo iliyofuata, timu ilicheza chini ya kiwango.

“Timu imekuwa ikicheza chini ya kiwango baada ya kupoteza mbele ya Mtibwa Sugar, hata tuliposhinda mbele ya Dodoma Jiji FC bado hakukuwa na kiwango bora.

“Kwenye mchezo wetu wa Jumatano dhidi ya Young Africans hali ilikuwa hivyo na tumepoteza hivyo makubaliano ya pande zote mbili tumefika makubaliano na kwa sasa Vivier Bahati atakuwa Kaimu Kocha Mkuu.” Alisema Thabit Zakaria.

Cioaba amekiongoza kikosi cha Azam FC msimu huu 2020/21 kwenye michezo 12, huku  kipata ushindi katika michezo 8 na kuambulia sare moja.

Kenya yarejesha masharti kudhibiti Covid 19
Pele: Tutacheza pamoja mpira juu mawinguni