Timu ya Azam FC ya Dar es salaam imetanguliwa nusu fainali kwa kuichapa Rhino Rangers ya Tabora.

Azam FC imechoza na ushindi wa mabao matatu kwa moja, katika.mchezo huo wa nusu fainali ya tatu uliochezwa Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Rhino Rangers ilitangulia kupata bao kupitia kwa Seleman Abdallah dakika 31 kabla Azam Fc hawajasawazisha kwa bao la Ayoub Lyanga dakika ya 33.

Kipindi cha pili Azam Fc walipata bao la pili kwa mkwaju wa penati iliopigwa na Agrey Morris dakika ya 65, huku bao la tatu na la ushindi likifungwa na mshambuliaji kutoka Zambia Obrey Chorwa Chirwa dakika ya 80.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kumsubiri mbabe wa mchezo wa nusu fainali ya nne itakayochezwa kuanzia saa moja usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya mabingwa watetezi Simba SC dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Timu nyingine zilizotinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ ni Young Africans baada ya kuifunga Mwadui FC mabao mawili kwa sifuri jana Jumanne mkoani Shinyanga, huku Biashara United Mara wakiivurumusha Namingo FC kwa mabao mawili kwa sifuri.

Young Africans watacheza nusu fainali dhidi ya Biashara United Mara mwezi ujao.

Ikumbukwe kuwa bingwa wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ‘CAFCC’ msimu ujao 2021/22.

Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara atapata fursa ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ‘CAFCL’ msimu ujao 2021/22.

Dodoma Jiji FC yadai kupuliziwa dawa chumba cha kubadilishia
Manara atuma ujumbe mzito mitandaoni