Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Azma FC Thabit Zakaria ‘ZAKAZAKAZI’ amesema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wa 18 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Young Africans utakaopigwa kesho Jumatano (April 05).

Azam FC itaikaribisha Young Africans katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es salaam ikiwa na lengo la kuzinyakua alama tatu muhimu, hatua ambayo italipa kisasi cha kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa. Azam FC ilipoteza dhidi ya Young Africans kwa mabao 2-0.

Thabit amesema wanatarajia mchezo wenye upinzani mkubwa kutoka kwa Young Africans ambayo kwa msimu huu imeonekana kuwa bora, lakini kwa upande wao wanaamini wapo imara zaidi kufuatia kuwa na kocha mwenye kutambua umuhimu wa mapambano na kusaka alama tatu muhimu.

“Kikosi chetu kimefanya maandalizi yake ya mwisho jana Jumatatu (April 03), Kocha ameniambia kila kitu kipo sawa na ana matarajio makubwa ya kuona mambo yakitunyookea, endapo wachezaji watafuata maelekezo yake kwa asilimia zote.”

“Niwaombe Mashabiki wa Azam FC kufika katika Uwanja wa wa Azam Complex bila kukosa na kuhakikisha wanakaa katika sehemu muhimu ambazo zitawasaidia kuishangilia vizuri timu yao yenye kiu ya mafanikio.” amesema ZAKAZAKAZI

Azam FC itashuka dimbani kesho Jumatano (April 05), ikiwa na alama zake 28, saba nyuma ya Simba SC iliyopo nafasi ya pili, huku Young Africans ikiongoza msimamo kwa kufdikisha alama 48.

Maajabu ya mwili wa Goonew kusimamishwa 'club'
Bashungwa afanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini