Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino Azam FC Thabit Zakaria (ZakaZakazi), amesema kikosi chao kinaendelea kujipanga kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Gwambina FC, utakaochezwa Jumatatu (Desemba 07) Uwanja wa Gwambina Complex.

Kikosi cha Azam FC kinaendelea na maandalizi ya mchezo huo Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Biashara United Mara ulioshuhudia kwa sare ya bao moja kwa moja siku ya Jumatatu (Novemba 30), mjini Musoma-Mara.

Zaka amesema makosa ambayo yalitokea kwenye mchezo wao dhidi ya Biashara United Mara yameanza kufanyiwa kazi na kaimu kocha mkuu Vivier Bahati, ili kupata matokeo kwenye mchezo dhidi ya Gwambina FC.

“Mchezo wetu uliopita tumegundua mengi ambayo tutayafanyia kazi kwani tulikuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda ila haikuwa hivyo zaidi wapinzani wetu walikuwa nao kwenye ushindani mkubwa,” amesema.

“Kwa sasa tupo Mwanza tutapambana kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu dhidi ya Gwambina. mechi sita zilizopita tumepata pointi tano tofauti na zile saba za awali ambapo tulipata pointi 21.” Amesema Zaka.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kucheza michezo 13, iliyowapa alama 26, huku ikifunga mabao 19.

Dawa tamu za HIV kuanza kutolewa kwa watoto
Lwanga mali halali Simba SC