Klabu ya Azam FC imetajwa na TFF kuwa klabu pekee iliyowasilisha vibali vya wachezaji wa Kimataifa iliyowasajili kwa msimu mpya wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa 2023/24.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo Jumatano (Agosti 09) imeeleza kuwa Azam FC imewasilisha vibali vya wachezaji 10 wa Kimataifa.

Wachezaji waliotajwa katika ripoti hiyo ni Ali Ahamada, Daniel Amoah, Kipre Junior, Prince Dube, Malickou Ndoye, ldrissu Abdulai, James Akamiko, Idiris Mbombo, Allasane Diao na Cheick Sidebe.

Klabu za Singida Fountain Gate, Simba SC na Young Africans bado hazijawasilisha vibali vya wachezaji wake wa kigeni.

“Hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kucheza mashindano ya Ngao ya Jamii kama hatakuwa amekamilisha taratibu za kisheria.” Imeeleza taarifa hiyo

Ikumbukwe kuwa Michuano ya Ngao ya Jamii inaanza rasmi leo Jumatano (Agosti 09) katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga, ambapo Mabingwa watetezi Young Africans watapapatuana na Azam FC, huku Simba SC ikitarajiwa kupambana na Singida Fountain Gate kesho Alhamis (Agosti 10).

Young Africans: Tumeona taarifa ya TFF, watacheza
Folarin Balogun athamilishwa Arsenal