Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imetangaza kuwa Kampuni ya Azam tayari imepewa leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kurusha matangazo ya chaneli za ndani bure.

Hayo yameelezwa na Naibi Waziri, Atashanta Nditiye leo, Mei 14, 2019 Bungeni jijini Dododma ambapo amesema Azam wapewa miezi saba kukamilisha mfumo wa kurusha bure chaneli za ndani hivyo wamewaomba watanzania kuwa na subiri kukamilisha taratibu hizo.

Nabu Waziri amesema hayo akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlalo Rashid Shangzi kutoka CCM, aliyehoji kwa nini Azam wananyimwa haki ya kuonyesha chaneli za ndani bure na kudai kuwa serikali inakiuka ibara ya 18 ya katiba ambayo inatoa haki ya kupata habari.

Aidha Agosti mwaka jana TCRA ilivifungia ving’amuzi vyote vinavyoonesha chaneli za ndani kwa kulipia na kuvitaka kurusha chaneli hizo bure suala ambalo lilipelekea baadhi ya ving’amuzi kufungiwa kuonyesha chaneli za ndani kwa kwenda kinyuma na leseni yao inayowataka kuonyesha chaneli hizo bure.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 15, 2019
Wanafunzi watumia chumba cha maabara kama darasa la kawaida