Kiungo Mshambuliaji kutoka Burkina Faso Stephane Azizi Ki ametamba licha ya kuonyesha uwezo mzuri akiwa na Young Africans msimu huu 2022/23, bado anaamini ana deni kubwa kwa mashabiki na wanachama, hivyo ameahidi kuonyesha uwezo wa juu zaidi msimu ujao wa 2023/24.

Nyota huyo pia amedadvua kuwa staili yake ya kushangilia kwa kunyoosha kidole juu inatokana na kumuonyesha Rais wa Yanga, Injinia Hers Said ambaye alimfuata mpaka nyumbani kwake kwa ajili ya kuhakikisha kuwa anajiunga na Yanga.

Aziz Ki kwa sasa amekuwa na msaada mkubwa ndani ya Young Africans tangu ajiunge nayo msimu huu akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast ambapo hadi sasa amefunga mabao tisa na kutoa pasi sita za mabao akiwa ndiye kinara wa pasi za mabao ndani ya Young Africans.

Aziz Ki amesema kuwa: “Nimekuwa nikifunga na kushangilia kwa staili ya kunyoosha kidole juu nikiwa ninamyooshea Injinia Hersi ambaye ni rais wa timu hii baada ya kunifuata nyumbani na kuzungumza na familia yangu kwa ajili ya kunisajili.

“Nataka nikuambie kuwa lile jambo watu wanaliona kama ni la kawaida lakini kwangu lile lilikuwa ni jambo kubwa na lenye maana kubwa sana, jambo ambalo nililiheshimu sana kiasi cha kutambua kuwa kulikuwa na dhamira ya dhati kati yangu na Young Africans.

“Hivyo nataka niwaambeie kuwa ninafuraha sana hapa Young Africans na jambo kubwa ni kwamba bado sijaonyesha uwezo mkubwa hivyo nitapambana kwa kuwa mwanzo wangu kwanza kucheza ndio na mara ya Tanzania, hivyo kuna vitu tayari nimeshavizoea naamini msimu ujao kuna mambo mengi zaidi watu wategemee kutoka kwangu,”

Chama aomba radhi Simba SC, atoa ahadi
Aishi Manula kupelekwa India