Licha ya kujiondoa kwenye harakati za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Gabon kwa kisingizio cha kukosa fedha, serikali ya nchini Chad imeamua kuidhamini klabu ya FC Metz inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa (Ligue 1).

Maamuzi ya serikali ya Chad yanachukua nafasi baada ya miezi mitano kupita tangu timu ya taifa hilo, ijiondoe kwenye Kundi G ambalo lilikua linajumuisha timu za Tanzania, Misri pamoja na Nigeria.

Klabu ya Metz imelitangaza taifa la Chad kama mdhamini wa jezi zao kwa msimu wa 2016/17.

Udhamini huo unaripotiwa kuwa wa thamani ya kiasi cha dola za Marekani milioni 17. 69

Licha ya pande zote kutoweka wazi thamani ya udhamini huo, serikali ya Chad imewaondoa hofu wananchi wake kwa kudai pesa hizo zimetoka kwa makampuni binafsi na ni matumizi yatakayoleta manufaa kwa taifa hilo masikini.

Chad ina matumaini udhamini huo utasaidia kuitangaza taifa lao na kuvutia watalii pamoja na kujenga taswira bora ya nchi hio mbele ya ulimwenguni.

Baada ya kufungwa na Tanzania bao 1-0 timu ya taifa ya Chad ilijiondoa katika mbio za Kusaka tiketi ya Fainali za Mataifa Afrika na kusababisha kundi G kubakiwa na timu tatu, Misri, Nigeria na Tanzania.

Furaha Ya Kufuzu Kwa AFCON 2017, Itakua Chungu Kwa Klabu Za Ulaya
Simba SC Yatoa Shukurani Kwa Mashabiki Wa Dodoma