Baada ya zaidi ya miaka 400, leo usiku, Sayari za Mshtarii (Jupiter) na Zohali (Saturn) zinatarajiwa kuonekana katika umbo moja kutoka Duniani.

Tukio hili linafanya Sayari hizo kuonekana kama ‘Nyota’ moja hii ikiwa ni mara ya kwanza tangu Julai 16, 1623 tukio kama hilo lilipoonekana kwa mara ya mwisho.

Si kwamba Sayari hizo zitakuwa kitu kimoja, bali zitakuwa katika mstari mmoja wa mwonekano kutoka Duniani.

Tafuta sehemu nzuri usiku wa leo utazame upande wa Kaskazini Magharibi.

Kesi ya Mwalimu aliyehukumiwa kunyongwa kuanza upya
Wivu wa mapenzi chanzo cha mauaji mengi nchini