Manchester United ikiwa nyumbani katika dimba la Old Trafford imefanikiwa kuichapa Benfica 2-0 na kwa mara ya kwanza ndani ya miaka minne United imepata nafasi ya kuingia katika hatua ya mtoano.

Anthony Martial, ambaye alikuwa tishio katika mchezo huo alikosa mkwaju wa penati baada ya kuangushwa katika eneo la hatari na Douglas na mkwaju wake kuchezwa na mlinda mlango wa Benfica Mile Svilar ambaye alikuwa katika kiwango kizuri.

Kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika United ilipata goli la kwanza baada ya mkwaju mkali wa Nemanja Matic kumgonga mgongoni mlinda mlango wa Benfica Mile Svilar na kutinga wavuni.

Kipindi cha pili dakika ya 78 Daley Blind aliifungia Manchester United bao la pili baada ya Marcus Rashford aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Jese Lingard kuangushwa katika eneo la hatari.

Kwa matokeo hayo Man U inaongoza ikiwa na alama 12, huku Benfica ikiburuta mkia na alama 0 baada ya kucheza michezo minne.

Chelsea yakiona cha moto ndani ya Stadio Olimpico
Lissu akunwa na Nyalandu, asema ni ujasiri wa hali ya juu