Baada ya shule kufungwa kwa zaidi ya mitano hatimae mamlaka ya Mji wa Wuhan china imetangaza kufunguliwa kwake septemba 1, jumanne.

Kiasi taasisi  2,842 za elimu , zenye  wanafunzi milioni 1.4 zinatarajiwa kufunguliwa na kuendelea na utaratibu wa masomo .Chuo kikuu cha Wuhani kufunguliwa siku ya jumatatu.

Mamlaka ya mji imesema kuwa bado inaendelea kuchukua taadhari dhidi ya ugonjwa huo huku wanafunzi wakielekezwa kuendelea kuchukua taadhari pamoja na kuvaa barakoa.

Wuhani eneo ambalo alipatikana mgonjwa wa kwanza wa COVID-19 , na eneo lililopata kuathirika zaidi na ugonjwa huo, tangu mei 18 haijaripoti kisa kipya cha ugonjwa wa COVID-19.

Wanaofanya ujangili kipindi cha kampeni watahadharishwa
Guillaume Soro aenguliwa kuwania urais