Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Zuwena Mohamed maarufu Shilole amezindua kitabu chake alichokipa jina la ‘’Broken Heart’’.

Kitabu hicho ambacho kimeandikwa na muandishi wa vitabu Jackson Fute kizinduliwa leo Agosti 28, 2018, Mlimani City jijini Dar es salaam.

Shilole hajaweka wazi amesheriki kwa kiasi gani katika uandishi wa kitabu hicho ambacho kinahusisha simulizi ya mapenzi, kikielezea namna mapenzi yanavyoweza kuteka hisia za mtu na kusababisha, uadui pindi mambo yanapokwenda ndivyo sivyo.

‘’Mwisho wa mahusiano tukaishia kuwa maadui wakubwa. Sikutaka kuiona sura yake tena’’ sehemu ya nukuu inayopatikana ndani ya kitabu hicho.

Mapema leo katika uzinduzi huo, Shilole ameshiriki katika zoezi zima la uuzaji wa kitabu hiko pamoja na kutia saini vitabu vilivyonunuliwa na mashabiki zake lakini pia Shishi alijichanganya na mashabiki wake kwa kupiga nao picha.

Shilole ni moja kati ya wanaewake wapambanaji sana hapa nchini, kwani juzi tu tumetoka kuona picha aliyoirusha mtandaoni ikionesha mjengo wake ambao hivi karibuni utaisha, ni uthubutu mkubwa ni mwanamke wa kuigwa kutokana na jitihada zake za kujituma kusaka maisha bora.

Kupitia akaunti yake ya instagram ametoa maelekezo namna ambavyo mtu anaweza kupata kitabu hiko cha ‘Broken Herat’ kwa wote waliopo Dar na mikoani.

 

 

Mtawa afariki dunia baada ya kujirusha kutoka Ghorofani
Vita dhidi ya ufisadi yapamba moto nchini Kenya