Zikiwa zimepita siku chache baada ya Mbunge wa Muleba kusini (CCM), Anna Tibaijuka kuaga Bungeni kama hatagombea tena uchaguzi ujao, Mbunge wa Bukoba Mjini (CHADEMA) Wilfred Lwakatare naye ameaga rasmi Bungeni kuwa hatagombea tena nafasi hiyo.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo, Aprili 14, 2020, alipokuwa anachangia katika hotuba ya bajeti ya mapato na matumizi ya wizara ya Tamisemi, na kusema kuwa anajivunia kwa uthubutu alioufanya kugombea kwa chama pinzani na kushinda.

Amesema katika utumishi wake alianza kufanyakazi Tamisemi kabla ya kugombea nafasi ya mwenyekiti wa mtaa na ilimpa ujasiri wa kugombea kupitia chama pinzani CUF ambapo alishinda ubunge.

” Najivunia sana kuwa upinzani na kuimarisha upinzani katika kipindi chote nilichokuwa mbunge na ndani ya upinzani, naondoka nikiwa na furaha na amani nikiomba Mbunge atakayekuja baada yangu aendeleze mafanikio haya” Amesema Lwakatare.

Naibu spika, Tulia Akson ambaye alikuwa anaongoza kikao ambemkumbusha Mbuge Lwakatare kuwa wapo wabunge ambao huwa wanaaga lakini ukifika wakati wa kuchukua fomu wanachukua na kugombea.

Watu wa India kuendelea kukaa Ndani hadi mwezi wa Tano
wananchi Tanzania kufundishwa kutengeneza barakoa (mask)