Hatimaye Miss Colombia, Ariadna Gutierrez ametoa fundo lililokuwa moyoni mwake kufuatia tukio tata la MC kumtangaza kuwa mshindi wa shindano la Miss Universe 2015 Jumapili iliyopita na baadae kuvuliwa taji hilo kwa madai kuwa tangazo hilo halikuwa sahihi, hivyo kuvuliwa taji na kumvisha Mrembo wa Ufilipino, Pia Alonzo Wurtzbach.

Mrembo huyo wa Colombia ametumia akaunti yake ya Instagram kufikisha ujumbe wake akieleza kuwa mtikisiko ule umekwisha na sasa muda tulivu umewadia. Mrembo huyo amesema anaamini hiyo ndiyo ilikuwa njia yake na kwamba ipo siku kilichofanyika kitajulikana wazi.

Miss Columbia alieleza kuwa mkanganyiko huo umepelekea nchi yake kutajwa kwa wingi kila kona ya dunia. Pia aliwapongeza wafilipino kwa ushindi walioupata.

Hivi ndivyo alivyoandika:
“After the storm comes the calm..I want to thank each and everyone of you who have sent messages of support and strength. Every one of you has become an incredible human being in my book and I am the most fortunate and thankful for having the support not only from one country but from the whole entire world.“Your destiny is written for you,”“And my destiny was this. I was able to bring happiness to my country after becoming Miss Universe for only a couple of minutes… Today because of that COLOMBIA and the LATIN COMMUNITY are being talked about in every corner of the world.”

Waongezewa Kifungo Baada ya Kushuti Video ya Rap Wakiwa Gerezani, itazame hapa
Rais wa Colombia Ahalalisha Matumizi ya Bangi, ataja sababu