Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema baadhi ya watoa huduma za afya wamekuwa wakiwasilisha madai yenye udanganyifu katika utoaji wa huduma kwa lengo la kujiongezea kipato kwa kutumia njia isiyo halali.

Dkt. Mollel amesema hayo hii leo Aprili 13, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Jesca Jonathan Msambatavangu kuhusu sababu zinazopelekea upotevu wa fedha katika vituo vya kutolea huduma za afya za mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) nchini.

Amesema, watoa huduma hao wamekuwa hawazingatia miongozo ya tiba nchini (STG) inayotolewa na Wizara ya Afya, kama ambavyo makubaliano baina ya pande zote yanavyoelekeza.

Aidha, Dkt. Molel ameitaja sababu nyingine kuwa ni kutozingatiwa kwa bei zilizoainishwa katika Mkataba wa Huduma baina ya Mfuko (NHIF) na Watoa Huduma.

Hata hivyo, katika hatua nyingine Dkt. Mollel amemuelekeza Mkurugenzi wa Bima ya Afya kuhakikisha ndani ya saa 24 watu wote wenye vigezo vya kupata huduma waanze kupata huduma hizo za CT-SCAN.

Olivier Giroud kusaini mmoja AC Milan
Mipango ya Kocha Robrtinho hadharani