Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamekutwa na mamilioni ya fedha majumbani kwao tofauti na kiwango cha mishahara yao.

Taarifa zilizotolewa na gazeti la Mtanzania zimeeleza kuwa Kitengo cha Uchunguzi, Jeshi la Polisi walifanya upekuzi kwa kushtukiza katika nyumba mbili za wafanyakazi wa shirika hilo ambao majina yao hayakutajwa na kuwakuta na mamilioni ya fedha.

Chanzo kililiambia gazeti hilo kuwa katika moja ya nyumba ya wafanyakazi hao iliyoko katika eneo la Salasala, Tegeta, Kinondoni, Dar es Salaam walikuta kiasi cha shilingi milioni 200 huku jirani yake akiwa na shilingi milioni 150.

“Walivamiwa wafanyakazi wawili (majina yanahifadhiwa), ambapo katika kila nyumba zilikutwa fedha nyingi. Kwa mtu wa kwanza zilikutwa Sh milioni 200 na yule wa jirani yake pia alikuwa na zaidi ya shilingi milioni 150,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, TRA juzi ilikanusha taarifa kuwa wafanyakazi wake hivi sasa wanafanya kazi kwa hofu kama inavyoelezwa na vyanzo mbalimbali.

 

Sugu Awataka Madiwani Wa Chadema Kufukuzana na ‘Kasi’ ya Magufuli
Lupita Nyong’o ‘Achemsha’ Kwenye Filamu Ya Star Wars, Muongozaji Ashindwa Kuvumilia