Baba mmoja anachunguzwa kwa tuhuma za kumng’ata na kumkwaruza kama paka mwanae mwenye umri wa chini ya miaka mitatu akidai kumfunza ujasiri ili asije kuwa na tabia za ushoga.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika eneo la Quiroga ndani ya jiji la Bogota nchini Colombia.

Vitendo hivyo vya kikatili vilibainika baada ya mama wa mtoto huyo kurudi nyumbani akitoka kazini na kumkuta mwanae akiwa na majeraha ya kushambuliwa. Mama huyo alipomuuliza mumewe kuhusu kilichomsibu mwanae, alicheka na kueleza kuwa alitaka kumfunza ukakamavu ili asije akawa shoga.

“He was laughing and teasing. He said that the boy had to be a man, that he couldn’t turn into a gay,” mwanamke huyo ameliambia Daily Mail ambalo limeyaficha majina ya wanafamilia hao.

Mwanamke huyo alieleza kuwa mwanaume huyo alifanya kitendo hicho tena mbele yake hali iliyomlazimu kuripoti Polisi. Hata hivyo, mwanamke huyo analilaumu Jeshi la Polisi Quiroga kwa kulipuuzia tukio hilo na kulipeleka kwa chama cha watumishi wa masuala ya jamii ambao wamepanga kumchukua mtoto huyo na kumlea.

 

Uhalifu: Wananchi wampiga Polisi na Kumpora bunduki
Lowassa ajifananisha na marais hawa, afuata nyayo za Maalim Seif