Mwanaume mmoja mwenye umri wa maiaka 56 raia wa Argentina aliyefahamika kwa jina la Domingo Bullicio, anatuhumiwa kumgeuza binti yake wa kumzaa kuwa mkewe na kuzaa naye watoto nane ndani ya kipindi cha miaka 22.

Antonio, ambaye ni binti wa mwanaume huyo amewaeleza polisi kuwa baba yake alimgeuza kuwa mkewe na kumtumikisha kingono tangu alipokuwa na umri wa miaka 9, mara baada ya mama yake kukimbia akiwa na watoto wengine watatu.

“Tangu mama yangu alipoondoka nyumbani, niligeuka kuwa mke wa baba yangu. Alinitumia vibaya tangu nikiwa na miaka nane. Alikuwa akinipiga na kunikimbiza na ukuni wa moto pale aliponiona nikizungumza na jirani. Alinitishia maisha kila siku na alinifanya nikae na hofu muda wote,” Antonio alielezea.

Alisema kuwa kutokana na mateso aliyoyapata kutoka kwa baba yake anataka haki itendeke na baba yake huyo aozee jela.

Mwanaume huyo alianza kukimbia hovyo baada ya Antonio mwenye umri wa miaka 37 hivi sasa, kutoa taarifa kwa vyombo vyenye mamlaka ya serikali . Polisi walifanikiwa kumkamata katika mji wa Loreto baada ya msako mkali uliochukua mwezi mmoja.

Serikali yalegeza masharti Bomoabomoa, Yamtimua Mwanasheria aliyemuokoa Lwakatare
Bulembo: BomoaBoa inamjengea Chuki Rais Magufuli Kwa Wananchi, isitishwe

Comments

comments