Baba mzazi wa Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa nyota wa Paris Saint-Germain, Neymar da Silva Santos Júnior, anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Brazil, kwa mujibu wa ripoti.

Inasemekana alikamatwa kutokana na uhalifu wa mazingira baada ya kudaiwa kufanya ukarabati kwenye jumba la kifahari la Neymar, ambalo limepigwa marufuku huko Mangaratiba Brazil.

Kama ilivyoripotiwa na Uol Sport, baba yake Neymar alikamatwa wakati wa operesheni iliyofanywa na wafanyakazi wa Jiji la Mangaratiba na kutoa mashtaka kwenye Jeshi la Polisi.

Baba huyo anayejulikana kwa jina la Neymar Sr, alikamatawa baada ya mabishano kutokea na Katibu wa Mazingira wa Mangaratiba, Shayenne Barreto.

Baba mzazi wa Mshambuliaji wa PSG Neymar Jr

Ripoti hiyo inaongeza Neymar Sr aliachiliwa, lakini waliosimamia operesheni hiyo walidai uchunguzi zaidi ufanyike.

Ikaelezwa sababu nyingine ya kukamatwa ni kutokana na kujenga ziwa la maji bandia ambalo limesababisha miti kukatwa na uharibifu mkubwa.

Taarifa imetolewa na idara hiyo huku ikitoa onyo: “Ujenzi umegeuka na kuharibu mazingira, umehamisha maji ya mto uliopo pembezoni mwa eneo hilo bila idhini, uchimbaji na usafirishaji wa mawe na miamba bila kutoa taarifa.”

Idara ya Mazingira ya Manispaa ya Mangaratiba inasemekana imeongoza shughuli zote na kuungwa mkono na polisi.

Taarifa hizi za baba yake Neymar ni siku chache tu baada ya mtoto wake kutuma barua ya kumuomba msamaha mpenzi wake Bruna Biancardi.

Wajane waitaka Serikali idhibiti msongo wao wa mawazo
Mifumo ya kieletroniki Serikali ya Zanzibar yazinduliwa