Baba mzazi wa Msanii wa Bongo Fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz, Faraji Nyembo amefunguka na kudai kuwa anatamani sana kwenda nchini Afrika ya Kusini kumuona mtoto wake ambaye sasa yupo chini ya uangalizi wa madaktari mara baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwekewa mfumo bandia wa kupitisha chakula.

Ommy Dimpoz amekuwa nchini Afrika kusini kwa miezi kadhaa kwa ajili ya matibabu.

Baba Dimpoz alipohojiwa amesema anatamani kwenda Afrika Kusini lakini kwa sasa hawezi kutokana na kukosa nauli ya kumfikisha huko.

‘’Namuombea mwanangu usiku na mchana ili Mungu amponye arudi kwenye muziki kama kawaida na kwa uwezo wake atapona, pia natamani sana kwenda kumuona lakini sina uwezo na naamini angeshangaa na angefurahi sana kuniona’’ amesema baba wa Ommy.

Aidha Ommy Dimpoz na baba yake hawana mahusiano mazuri kutokana kwamba siku za huko nyuma mwanababa huyo alimtelekeza mwanaye katika maisha magumu na kwenda kula bata nchi za nje.

Ommy amekuwa akisumbuliwa na tatizo la koo la chakula ambalo liliziba hali iliyopelekea ashindwe kupitisha chakula wala maji, kwa mujibu wa madaktari tatizo hilo limetokana na sumu ambayo inasemakna Ommy alikula bila kutambua.

Hivyo Ommy anaendelea vizuri kiafya mara baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa uliopelekewa kumuwekea koo jingine la chakula ili aweze kula kunywa kama binadamu wengine wa kawaida.

Wanafunzi wa Darasa la Saba mkoa wa Simiyu wateta na RC Mtaka
Video: Matukio ya ukatili kwa Wanawake na Watoto yameongezeka- LHRC