Baba mzazi wa Marehemu Steven Kanumba anayefahamika kwa jina la Charles Kanumba amesema kuwa ameota ndoto kuhusu maamuzi ya Mahakama dhidi ya Elizabeth Michael maarufu kama Lulu.

Baba Kanumba amesema kuwa amekuwa akioteshwa kuhusu uamuzi wa Mahakama na kwamba aliota Lulu ataachiwa huru.

Ameeleza kuwa kwa kifungo cha miaka miwili kwa kosa hilo ni adhabu ndoto inayofanana na ndoto yake ya kuachiwa huru. Hata hivyo, amesema kwakuwa amesikia mawakili wanaomtetea Lulu watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, anaamini ndoto yake itatimia kwani ataachiwa huru.

“Nimekuwa naoteshwa, na kila nachokiota kinakuwa kweli. Nimesikia wanakata rufaa, na wakikata rufaa lazima Lulu ataachiwa. Nimeshaoteshwa kuhusu hilo,” Baba Kanumba ameiambia Amplifaya ya Clouds FM.

Alisema kuwa anaamini mtu anapofikishwa Mahakamani, Mahakama itatenda haki na ndicho alichokuwa anatarajia.

Lulu amehumiwa kifungo cha miaka miwili jela leo baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake.

Wakili Peter Kibatala anayemtetea Lulu ameeleza kuwa watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 14, 2017
Chris Brown aweka rekodi na ‘Heartbreak on Full Moon’