Baba wa kambo wa Kim Kardashian, Caitlyn Jenner aliyejibadili kuwa mwanamke ametajwa kushindania tuzo ya bibi/babu bora wa mwaka 2015.

Tuzo hiyo inatolewa na mgahawa maarufu nchini Uingereza wa Chain TableTable ambao umeendelea kuwahamasisha watu mbalimbali kuwapigia kura washiriki wanaowapenda.

Akizungumzia sababu za kuanzisha tuzo hiyo, Meneja masoko wa mgahawa huo, Jo Watling alisema kuwa lengo la kuanzisha tuzo hiyo ni kuhakikisha wanatambua mchango wa wazee katika ngazi za familia.

Malkia Elizabeth na Caitlyn wameingia fainali za mashindano ya tuzo hizo kwa kupigiwa kura nyingi.

Mgomo Wa Walimu Wafunga Shule Zote Kenya
H Baba Ampa Mwanae Zawadi Ya Kiutuuzima