Mchezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 20 kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 2017, Oluwaseyi Babajide “Sheyi” Ojo, ana ndoto za kurejea barani Afrika na kulitumikia taifa la Nigeria, ambapo ndipo asili ya wazazi wake.

Ojo, ambaye kwa sasa amepelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Reims ya Ufaransa akitokea Liverpool, amesema anafikiria kufanya maamuzi ya kuondoka England, kutokana na kuamini hatokua na nafasi ya kucheza katika timu ya taifa ya wakubwa ya nchi hiyo miaka ya usoni.

Amesema haoni kama atapata nafasi hiyo kutokana na kuwa na wakati mgumu wa kucheza mara kwa mara katika kikosi cha Liverpool, ambacho kwa sasa kimesheheni wachezaji wengi kutoka nje ya England wanaocheza nafasi ya ushambuliaji.

Hata hivyo amedaI hafahamu lolote kuhusu soka la Nigeria, lakini anatambua ndipo wazazi wake walipotokea, na endapo viongozi wa shirikisho la soka nchini humo (NFF) watamuita, atakua radhi kujiunga na The Super Eagles.

“Kwa kweli sihafahamu lolote kuhusu Nigeria, nimekua naifuatilia katika televisheni na kuona soka lao linalovutia, wakinihitaji nitakua tayari kuondoka England na kujiunga nao,” alisema Ojo alipohojiwa na shirika la utangazaji la Uingereza (BBC).

“Natambua ni taifa kubwa kisoka katika ukanda wa bara la Afrika, wanafanya vizuri na wameshashiriki fainali za kombe la dunia zaidi ya mara tatu, ninawafuatilia sana.

“Wazazi wangu asili yao ni Nigeria, leo nikipata nafasi ya kuitumikia Super Eagles nitajihisi furaha, maana nitakua ninalitumikia taifa la wazazi wangu,” alisema.

Kwa sheria na kanuni za FIFA, Ojo ana nafasi ya kuihama England na kujiunga Nigeria, kutokana na kutokua na kizuizi chochote cha kufanya hivyo, kwani mpaka sasa hajawahi kuitwa na kuichezea timu ya taifa ya wakubwa ya The Three Lions (England).

Akiwa na timu za taifa za vijana za England kuanzia miaka 16 hadi 21, Ojo ameshacheza michezo 43.

Mfanyakazi amtuhumu Beyonce kwa Uchawi
Iran yaahidi kisasi kwa Marekani, Israel kwa shambulizi la gwaride