Afarah Suleiman, Babati – Manyara
Mkuu wa Wilaya ya Babati, Lazaro Twange kwa kushirikiana na Wananchi wa kata ya Singu pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya mji wamefanya usafi wa mazingira katika mpaka wa Halmashauri ya mji na Halmashauri ya Wilaya huku akiihimiza jamii kutunza mazingira yanayowazunguka.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Twange amesema pia Wananchi mbali na usafi wa kila jumamosi pia wanatakiwa kupanda miti, ili kuufanya mji wa Babati kuwa safi katika kata zote nane za Halmashauri na kuendelea kuongoza katika nyanja za usafi Nchini.
Awali, Mkurugenzi wa Mji wa Babati, Pendo Mangali alisema kutokana na agizo la Mkuu wa mkoa Manyara la usafi katika maeneo mbalimbali, wameona ni vyema kuanza kufanya usafi huo kwa kuanzia mpaka wa Halmashauri ya Mjini na Vijijjini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji na zoezi hilo ni endelevu.
Kwa upande wao Wananchi na Watumishi wa Halmashauri hiyo, wamesema zoezi hilo linaleta ushirikiano pamoja na kufanya mazingira kuwa safi na ni hamasa kwao wengine ambao hawajapata nafasi ya kushiri ili wakati waweze kushiriki na kuhimiza uachaji wa mara moja wa kutotupa taka hovyo na kuchukua tahadhari ya uwepo wa mvua ya El-nino.