Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limemkamata Mzee Said Abduratifu Tumain (67) kwa tuhuma ya kumbaka na kumpa ujauzito mjukuu wake (13) mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kizigo Manispaa ya Tabora

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Barnabas Mwakalukwa amesema Mama mzazi wa mtoto ndiye aliyegundua mabadiliko ya mtoto

Jeshi la Polisi Mkoani hapo limefanikiwa kumnasa mtuhumiwa huyo ambae ni mganga katika manispaa hiyo kwa kushirikiana na wananchi.

Hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limewahasa wananchi kuendeelea kutoa ushirikiano na polisi kwa kutoa taarifa kwa vitendo viovu.

Jela miaka miwili kwa kuisababishia hasara TCRA
Rais Magufuli afanya uteuzi,amrudisha Mwakyembe