Kufuatiwa na kifungo cha maisha alichohukumiwa Nguza Viking maarufu kama Babu Seya katika gereza la Ukonga wilaya ya Ilala jijini Dar es salaa, siku za karibuni kumesambaa habari potofu zikisema Babu Seya ameandika waraka mzito kwa Rais Magufuli akimuomba amtenganishe na maisha ya gereza.

Maandiko hayo yalikanushwa na Babu Seya akisaidiana na Mkuu wa Gereza, ACP Stephen Mwaisabila ambaye amekiri kuwepo kwa taratibu maalumu za wafungwa kuandika barua kwa kiongozi yeyote mkubwa na kukanusha kuwa ujumbe uliosambaa haukuandikwa na Babu Seya.

“Inashangaza kuona kuna watu wanafanya kitu kwa wafungwa kuandikia uzushi mbalimbali kuhusu Babu Seya”.

Hata hivyo Babu Seya mwenyewe alipata nafasi ya kuzungumza na chombo cha habari kilichomtembelea siku hiyo na kukanusha kuhusu taarifa zilizokuwa zikienea kwenye mitandao ya kijamii.

“Ujumbe unaoenea kwenye mitandao ya kijamii, sijauandika ila nafarijika kuona kuna watu wananipigania’’ amesema babu Seya.

Aidha alichukua nafasi hiyo kumuomba Rais Magufuli alipitie faili lake upya kwani anaamini hana hatia yeyote.

Baadhi ya maandiko yaliyosadikia kuandikwa na babu Sea ni “Mwambieni rais nimeiweka akiba yangu ya tumaini la mwisho kwake,yeye ni wa pili aweze kunitenganisha mimi na maisha ya gereza,
“Sipendi ndoto yangu ya kuja kufia gerezani…naichukia kama tawala za Herode pale Galilaya. Naumwa huku hakuna makaburi mazuri ya kuzikia wafu wetu”.

 

Azam yajinoa vikali kuikabili Mbao Fc
Wolper aupa kiki wimbo wa Harmonize 'Shulala'