Meneja wa Diamond Platinumz, Babu Tale amesafisha hewa na kumtetea mwimbaji huyo kuhusu kauli iliyokaririwa na vyombo mbalimbali vya habari alipokuwa anaongea na TBC FM kuwa yeye ndiye anayeidhinisha nyimbo za wasanii wa Tanzania kuchezwa MTV.

Akiongea na XXL ya Clouds Fm, Babu Tale amesema kuwa watu walioandika kauli hiyo walikosea kwa kuwa Diamond hakumaanisha wala kutamka kama ilivyoandikwa.

“Diamond aliulizwa ‘wasanii gani ambao amewasaidia na anasupport vipi muziki wa nyumbani kwenda nje’, akajibu, ‘mimi mbona huwa nasaidia watu wengi? na kuna kipindi mtu huwa ananipigia simu kuuliza unamjua flani? ni mzuri? kuna media za nje huwa zinanipigia kuuliza kama namjua flani?’… hivyo tu na yeye huwa anasema mzuri ili Watanzania wapae,” alisema Babu Tale.

Picha: Mchungaji amchoma moto muumini akidai amesikia sauti ya Mungu
Rais Wa Soka La Barani Asia Atembelea Wizarani