Mchungaji Ambikile Mwasapile maarufu kama ‘Babu wa Loliondo’ amesema ameoteshwa kuwa maelfu ya watu watafuata tiba yake maarufu ya ‘Kikombe cha Babu’ anayoamini inatibu magonjwa mengi.

Mwaka 2011, maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa kisiasa, watu maarufu, wafanyabiashara wakubwa na wananchi kwa ujumla walifurika katika kijiji  cha Semunge kupata tiba hiyo.

Akizungumza juzi Jumapili mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda alisema kuwa ameoteshwa kama ilivyokuwa mwaka 2011 kuwa watu kutoka ndani na nje ya nchi wataifuata tiba hiyo kwa gharama ileile ya shilingi 500.

Amesema kuwa hadi sasa anaendelea kutoa tiba hiyo kwa watu wachache wakiwemo watalii ambao wamemueleza kuwa walipata habari za tiba hiyo wakiwa nchini Ulaya, hivyo anaandaa miundombinu ikiwa ni pamoja na kujenga vibanda zaidi.

Naye Naibu Waiziri aliyepata pia kikombe, alimshukuru kwa kusababisha maendeleo zaidi ya kijamii katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na miundombinu.

Kutokana na tiba hiyo, wananchi wengi katika eneo hilo wamepanda miti inayotoa dawa hiyo hali inayosababisha pia kuchagiza utunzaji wa mazingira, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ngorongoro, Raphael Siumbu.

Video: UN, Kenya walaani mauaji askari wa JWTZ
Polepole asema Lowassa alishindwa kumshawishi Kikwete kuhusu Babu Seya