Baada ya kukubali kichapo cha mabao mawili kwa sifuri kutoka kwa wagonga nyundo wa jijini London West Ham Utd, meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameshindwa kumlaumu mlinda mlango Petr Cech, ambaye alionekana kuwa chanzo cha kipigo hicho.

Wenger, alikataa kuziamishia lawama za kupoteza mchezo huo wa kwanza wa ligi msimu huu, kwa mlinda mlango huyo aliyemsajili akitokea Chelsea katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi, kwa kuamini hakupaswa kufanyiwa hivyo.

Babu huyo wa kifaransa amesema, kwa ujumla kikosi chake hakikucheza vizuri na kama itamlazimu kulaumu, basi atawalaumu wachezaji wote ambao jana aliwapa nafasi ya kucheza kwa lengo la kuzisaka point tatu muhimu.

Amesema, haipendezi kwa mtu kulaumiwa pekee yake, kutokana na hali halisi ya mchezo wa soka ambao hutafsiri makossa kwa ujumla wa timu nzima na si kumtazama mmoja mmoja.

Cech, alionekana kutokua katika kiwango chake katika mchezo huo na kusababisha mabao waliyofungwa Arsenal kuingia langoni mwake kwa urahisi.

Mlinda mlango huyo kutoka jamuhuri ya Czeh, alisajiliwa na Arsenal kwa ada ya uhamisho wa paund million 10 akitokea Chelsea, ambapo alikua hana nafasi ya kucheza mara kwa mara kufuatia uwepo wa mlinda mlango kutoka nchini Ubelgiji, Thibaut Courtois.

Mabao ya West Ham Utd katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Emirates yalifungwa na Cheikhou Kouyate pamoja na Mauro Zarate.

CCM Yapasuka Arusha
Sammata Na Ulimwengu Kuwakabili Azam FC