Beki Shkodran Mustafi anatarajia kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoondoka kaskazini mwa jijini London yalipo makao makuu ya klabu ya Arsenal, kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwishoni mwa juma hili.
Mustafi ambaye alitumika kama mchezjai wa akiba wakati wa mchezao wa ligi ya England dhidi ya Liverpool hapo jana, anawaniwa na klabu ya Inter Milan ya nchini Italia, ambayo imeonyesyha nia thabiti ya kumsajili.
Beki huyo kutoka nchini Ujerumani alijiunga na The Gunners msimu uliopita akitokea Valencia CF, lakini Arsene Wenger yupo tayari kumuachia katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.
Pamoja na kumuuza Gabriel Paulista kwenye klabu ya Valencia CF ya Hispania mapema mwezi huu, mzee huyo wa kifaransa bado anaamini kuondoka kwa Mustafi hakutomuathiri chochote kwa msimu huu, kutokana na hali ya Per Mertesacker kuendelea kuimarika.
Uwepo wa beki kinda Rob Holding, nao unatajwa kumpa kiburi mzee huyo, kwa kuamini safu yake ya ulinzi itaendelea kuimarika.