Kocha Badru Mohamed ameanza kazi rasmi ya kukonoa kikosi cha Mtibwa Sugar, ikiwa ni saa chache baada ya kuthibitika ameachana na Gwambina FC ya mkoani Mwanza.

Kocha Badru alionekana kwa kazini jana Jumatatu (Mei 17), akikinoa kikosi cha Mtibwa Sugar ambacho kina wakati mgumu wa kuhakikisha kinasalia kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 15 ikiwa imekusanya jumla ya alama 31 baada ya kucheza jumla ya michezo 29.

Kocha huyo ameiacha Gwambina FC ikiwa nafasi ya 17 baada ya kucheza jumla ya michezo 28 lakini hakuanza msimu na timu hiyo ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mchezo wake wa mwisho ilikuwa ni mbele ya JKT Tanzania, Uwanja wa Gwambina Complex na timu yake ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Kocha Badru anatarajiwa kuwa kwenye benchi la ufundi la Mtibwa Sugar leo Jumanne (Mei 18) katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo kikosi chake kitapambana dhidi ya Mbeya City FC, katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kikosi cha Mtibwa Sugar kwa muda wa miezi kadhaa kimekuwa kikinolewa na kocha msaidizi Vicent Barnabas, bada ya Kocha Mkuu Hitimana Thiery kugoma kurejea klabuni hapo, kwa madai ya kushindwa kutimiziwa taratibu za kazi yake kikamilifu.

Serikali yajipanga kukabiliana na ujambazi mitandaoni
Wachezaji KMC FC wapewa mapumziko