Afrika Kusini (Bafana Bafana) iliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia uliopigwa mjini Johannesburg.

Percy Tasu aliwapatia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 1 kabla ya Themba Zwane kuongeza bao la pili dakika ya 33 na Sibusizo Vilakazi kufunga bao la tatu kipindi cha kwanza kikimalizika kwa Afrika Kusini kuwa mbele kwa mabao 3-0.

Katika mchezo huo mchezaji wa Africa kusini alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 69 lakini mpaka dakika 90 zinamalizika wenyeji waliibuka na ushindi wa 3-1 bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Burkina Faso lilifungwa na Alain Traore.

Uganda ilitoka sare tasa na Ghana

 

Kwengineko Uganda wakicheza katika uwanja wanyumbani wa Nelson Mandela mjini Nambole dhidi ya Ghana ‘Black Stars’ walitoka sare ya 0-0 matokeo ambayo matokeo ambayo yanapunguza matumaini yao ya kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Urusi 2018.

Lema: Hakuna jipya baraza la mawaziri
Video: Lissu afanyiwa upasuaji wa 15, JPM ajipanga upya