Mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint – Germain (PSG) wapo tayari kuweka mezani kitita cha paundi million 18 kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Swansea City, Bafetimbi Gomis, hii ni kwa mujibu wa Sky Sports.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Ufaransa ameingia katika rada za PSG iliyodhamiria kuendelea kutetea taji la ligi kuu (League 1).

Harakati za uhamisho wa Bafetimbi zinatiwa nguvu na taarifa za kiwango kimewavutia baadhi ya mawakala wa klabu mbalimbali barani Ulaya.

Tayari PSG wameteta na wakala wa nyota huyo pamoja na klabu yake ya Swansea City, ambapo wamethibitisha kuwepo kwa mipango ya kuuzwa kwa Bafetimbi.

PSG walimthaminisha Mfaransa huyo kwa dau la paundi million 18 ingawa wameonyesha dalili za kukubali kushusha kiwango.

Swansea pamoja na kuweka bayana thamani ya mchezaji huyo, wamethibitisha kuwa Bafetimbi ni miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa na klabu mbalimbali za barani Ulaya.

“Bafetimbi anawindwa na timu nyingi za Ulaya, lakini nataka acheze katika kikosi ambacho atapambana na kudumu.” “Ni mchezaji mwenye ofa nyingi, ila ni jambo la kusubiri kuona ifikapo kipindi cha usajili kikifika mwisho.” Tovuti ya klabu ya Swansea City iliandika

 

Alex Sandro Lobo Silva Ajipigia Debe Kwenda Man City
Kikwete atunukiwa shahada ya udaktari wa falsafa