Kocha wa timu ya taifa ya Ivory Coast Ibrahim Kamara amemuita beki wa klabu ya Manchester United Eric Bailly kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo, ambacho kitacheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afika dhidi ya Guinea mwishoni mwa juma lijalo.
Beki huyo ametajwa kwenye kikosi cha Ivory Coast, huku akikabiliwa na changamoto ya kutokuchezwa kwa kipindi kirefu akiwa na klabu yake ya Man Utd, ambapo kwa mara ya mwisho alionekana kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Newcastle United uliochezwa Oktoba 06.
Hata hivyo katika mchezo huo uliomalizika kwa Man Utd kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa mawili Bailly alicheza kwa dakika 19 pekee, kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine.
Kocha Kamara pia amemuita kiungo mshambuliaji Souleymane Doumbia, ambaye ni mzaliwa wa Ufaransa, kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Ivory Coast ambacho kitalazimika kushinda mchezo dhidi ya Guinea.
Guinea inongoza msimamo wa kundi H kwa kufikisha alama 10, ikiwa ni alama tatu zaidi ya Ivory Coast huku Jamuhuri ya Afrika ya kati watakaocheza na Rwanda wakiwa na alama nne.
Kikosi cha Ivory Coast kitakachoikabili Guinea.
Makipa: Sylvain Gbohouo (TP Mazembe, DR Congo), El Hadje Moustapha Dante (LYS Sassandra) na Ali Badra Sangare (Free State Stars, South Africa)
Mabeki: Eric Bailly (Manchester United, England), Serge Aurier (Tottenham Hotspurs, England), Mamadou Bakayoko (Mechelen, Belgium), Ghislain Konan (Reims, France), Wilfred Kanon (ADO Den Haag, Netherlands), Jean Philippe Gbamin (Mainz 05, Germany), Souleymane Doumbia (Grasshoppers, Switzerland) na Cheick Comara (Wydad Athletic Club, Morocco)
Viungo: Jean Michel Seri (Fulham, England), Serey Die (FC Basel, Switzerland), Franck Kessie (AC Milan, Italy), Cheick Doukouré (Levante, Spain), Victorien Angban (FC Metz, France) na Yacou Méïté (Reading, England)
Washambuliaji: Jonathan Kodjia (Aston Villa, England), Roger Assale (Young Boys, Switzerland), Nicolas Pepe (Lille, France), Max Gradel (Toulouse, France), Vakoun Bayo, (Dunajská Streda, Slovakia) na Wilfred Zaha (Crystal Palace, England)