Beki wa pembeni wa klabu ya Everton, Leighton Baines atashindwa kujumuika na wachezaji wenzake klabuni hapo, kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo kufuatia majeraha yanayomkabili kwa sasa.

Meneja wa klabu ya Everton, Roberto Martinez amethibitisha taarifa hizo kwa kusema Baines, alishindwa kucheza mchezo wa ufunguzi wa ligi ya msimu huu, kufuatia majeraha ya kifundo cha mguu yanayomkabili na imebainika anahitaji kufanyiwa upasuaji.

Martinez, amesema kuumia kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 30, ni pigo kubwa kwa kikosi chake ambacho kimeweka dhamira ya kweli ya kupambana masimu huu na kumaliza kwenye nafasi nzuri, kama si kutwaa ubingwa wa England.

Amesema kwa kipindi cha miezi mitatu sawa na majuma 12-13, mchezji huyo atakosa zaidi ya michezo 12, hivyo hana budi kujipanga kikamilifu ili kufanikisha mipango mbadala itakayoweza kumsaidia.

Kuumiwa kwa Baines, pia ni pigo kwa timu ya taifa ya England, ambayo mwanzoni mwa mwezi ujao itakuwa na changamoto ya kupambana kwenye harakati za kusaka nafasi ya kushiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya, dhidi ya San Marino na Uswiz.

Michezo mingine Baines atakayoikosa kwa upande wa timu ya taifa, itakua dhidi ya Estonia pamoja na Lithuania itakayochezwa mwezi Oktoba.

Harakati Za Usajili Barani Ulaya
Ni Vita Kati Ya Stefan Effenberg Vs Hughes, Shaqir