Kocha Mkuu wa Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’, Bakari Shime ana matumaini ya kuendeleza ubabe katika mchezo wa Mkondo wa Pili wa kusaka tiketi ya kushiriki Michezo ya Olimpiki dhidi ya wapinzani wao Botswana.

Mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam juma hili, Twiga Stars ilichomoza na ushindi wa 2-0, na kujiweka katika mazingira mazuri kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa Oktoba 31, mwaka huu jijini Gaborone.

Kocha Shime amesema anatarajia upinzani mkali kutoka kwa Botswana kwenye mchezo wa Mkondo wa Pili kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza, kwa sababu wapinzani wao wanajua kupambana na hawakati tamaa.

“Ninatarajia upinzani mkubwa kutoka kwa wapinzani wetu watakapokuwa nyumbani, tunakwenda kucheza na timu inayojua na haikati tamaa mapema, hivyo nimejipanga kuhakikisha tunaendeleza ushindi katika uwanja wa ugenini.”

“Lengo ni kuhakikisha tunasonga mbele katika harakati za kuwania kucheza Michuano ya Olimpiki, nina imani kubwa na wachezaji wangu watapambana, lakini tunachokihitaji kwa watanzania ni kuendelea kuwa na sisi.” amesema Shime.

Wadakwa wakisafirisha Mifugo Nje kimagendo
Kevin De Bruyne kuvutwa Saudi Arabia