Kumekuwa na hali ya sintofahamu katika klabu Chelsea iwapo kocha wa klabu hiyo, Antonio Conte atasalia au ataondoka baada ya msimu wa ligi kuu ya Uingereza 2018/2019 kumalizika hasa kutokana na Chelsea kushindwa kutetea ubingwa wa ‘EPL’.

Licha ya Chelsea kutinga fainali ya kombe la ‘FA’ bado matumaini ya klabu hiyo kumaliza katika nafasi nne za juu yameonekana kugongwa mwamba jambo linalozua hofu ya kutimuliwa kwa kocha Antonio Conte kutokana kushindwa kuipeleka Chelsea kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Kiungo wa klabu hiyo mfaransa Tiemoue Bakayoko amesema atasikitika iwapo Conte ataondoka kwani anafurahia kuwa chini ya kocha huyo na ndani mwaka mmoja amemsaidia kuboresha kiwango chake.

Kiungo huyo aliyesajiliwa kwa kiasi cha Paundi milioni 40 kutoka katika klabu ya Monaco msimu uliopita, amesema Conte hajawaambia wachezaji kitu chocote kuhusu hatma yake ndani ya klabu ya Chelsea na mara zote amekuwa akipambana kuhakikisha timu yake inapata ushindi na kufanya vizuri msimu huu.

”Kama mchezaji nisingefurahia kuona kocha akiondoka, kila mmoja anapenda kufanya kazi, kuwa na mahusiano na kocha kwa muda mrefu”, alisema Bakayoko.

Chelsea wapo katika nafasi ya 5 wakiwa na pointi 70 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza huku wakiwa wametinga fainali ya kombe la FA ambapo watakutana na Manchester United katika mchezo wa fainali utakaopigwa tarehe 19 Juni kwenye uwanja wa Webley.

 

 

 

Zari alichowashauri wanaume wanaochepuka
Seleman Nonga, Dadu Fadhil Msemo waondolewa RCL