Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), limesema kuwa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli alikuwa mzalendo wa kweli katika kupanua wigo wa Kiswahili na kwamba walimuona kama mkombozi wa kukibeba na kukipeleka Kiswahili mbele zaidi.

Akizungumza na Dar24 Media katika kipindi cha mahojiano Ambroce Mghanga, Mchunguzi Lugha Mwandamizi wa Lugha ya Kiswahili BAKITA, amesema kuwa Hayati Magufuli alikuwa na nia ya dhati ya kuifanya lugha ya kiswahili itambulike kama lugha ya kimataifa na hata kutumika mpaka kwenye mikutano ya SADC.

Mghanga amesema matumizi ya lugha ya Kiswahili SADC ni jambo la kujivunia kwenye ukuaji wa Kiswahili, kwa kuwa limeleta fursa kwa Nchi ya Tanzania kutokana na uhitaji wa walimu zaidi, wataalamu wa Kiswahili, Wakalimani, lakini pia ongezeko la utungaji wa vitabu vya Kiswahili.

Kuhusu hofu ya utoshelezaji wa Msamiati katika lugha ya Kiswahili, Mghanga amesema kuwa hakuna lugha inayojitosheleza duniani kwani lugha zote zinategemeana kwa kutohoa maneno.

Aidha, Mghanga amewaasa Watanzania kuwa wazalendo na kutumia lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo lugha mama kwani kiswahili ndio lugha iliyotumika Tanzania kupata Uhuru, na kutaka itumike pia sasa kukomboa watanzania kifikra na kuleta maendeleo.

Mwakalebela afungiwa miaka 5
Ibenge: Nitaifunga Simba SC kwa Mkapa